IQNA

Maqarii wengine 3 Wairani ni miongoni mwa waliokufa shahidi Mina

6:49 - October 02, 2015
Habari ID: 3377233
Maqarii wengine watatu wa Qur'ani Tukufu Wairani wametambuliwa kuwa miongoni mwa Mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina Alhamisi wiki iliyopita.

Idara ya Hija ya Iran imetangaza majina ya maqarii hao Wairani walipoteza maisha Mina kuwa ni Hassan Danesh, Foad Mash’ali and Saeed Saeedizadeh.
Awali walithibitishwa kufa shahidi maqarii wengine wawili Wairani ambao ni Mohsen Hajihassani Kargar and Amin Bavi.
Kwa maelezo hayo ni maqarii watano Wairani  walipoteza maisha katika maafa ya Mina tarehe 24 Septemba wakitekeleza amali za Hija katika siku kuu ya Idul Adha.
Kwa ujumla Mahujaji 465 Wairani wamethibitishwa kupoteza maisha katika maafa hayo ambapo inaaminika Mahujaji waliopoteza maisha ni zaidi ya elfu tano.

captcha