IQNA

Kampeni ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

22:53 - April 21, 2016
Habari ID: 3470261
Kundi la wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Uingereza limeanzisha wimbi kubwa la malalamiko katika mitandao ya kijamii likitaka kuachiwa huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky

Wanaharakati hao wamesema kuwa, wana matarajio kwamba kwa kutumia mitandao ya kijamii, watafanikiwa kuwaamsha walimwengu kuhusu masaibu na ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Nigeria dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.

Wanaharakati hao wa kutetea haki za binadamu wanasema kuwa, wimbi hilo la malalamiko ni utangulizi wa kuilazimisha serikali ya Abuja imwachie huru Sheikh Zakzaky.

Kumekuwepo wasiwasi mkubwa kuhusu ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Nigeria dhidi ya Waislamu hususan wafuasi wa Ahlul Bait nchini humo. Miezi kadhaa iliyopita jeshi la serikali ya Nigeria lilishambulia kituo cha kidini cha Waislamu hao na kuua mamia miongoni mwao katika mji wa Zaria. Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na wenzake kadhaa pia wangali anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa miezi kadhaa sasa.

3490843

captcha