IQNA

Mwanachuo wa Uingereza: ISIS si Uislamu

12:55 - July 12, 2016
Habari ID: 3470448
Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu Uingereza ametoa taarifa na kusema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh halina uhusiano wowote na Uislamu.
Mwanachuo wa Uingereza: ISIS si Uislamu

Katika taarifa, Toni Jones, mwanafunzi wa taaluma ya sheria katika Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland ameashiria hujuma za kigaidi katika Msikiti wa Mtume SAW, Al-Masjidan-Nabawi, mjini Madina mnamo Julai 4, na kabla ya hapo hujuma za kigaidi Baghdad, Dhaka na Istanbul na kusema hujuma hizo zote, ambazo ISIS ilidai kuhusika nazo, zimefanyika katika nchi za Kiislamu. Amesema kuna dhana potovu kuwa ISIS ni kundi la kigaidilinalpigana kwa niaba ya Uislamu. Mwanachuo huyo wa Scotland amesema wengi hawafahamu kuwa, tokea kuibuka kwake, ISIS imewaua Waislamu wengi zaidi ya wasiokuwa Waislamu. Ameongeza kuwa, ukweli huu unapuuzwa na wengi wakati hujuma ya kigaidi inapojiri katika miji ya nchi za Magharibi.

Ameashiria ripoti ya mwaka 2009 ya Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha Westpoint ambayo ilibaini kuwa watu waliouawa na kundi la al Qaeda, ( ambalo ni chimbuko la ISIS), kati ya mwaka 2004 na 2008 ni asilimia 12 tu waliokuwa raia wa nchi za Magharibi, jambo ambalo linamaanisha kuwa al Qaeda iliua Waislamu mara saba zaidi ya wasiokuwa Waislamu.

Kuhusiana na ISIS ukweli ni huo huo. Katika mwaka 2016 pekee, ISIS imetekeleza hujuma za kigaidi 21 na 18 kati yazo zimetekelezwa katika nchi zenye Waislamu wengi hama vile Iraq, Syria, Saudi Arabia na Uturiki. Aidha watu waliouawa na ISIS katika nchi zisizo za Kiislamu hadi kufikia sasa katika mwaka 2016 ni 83 katika hali ambayo Waislamu zaidi ya 677 wameuawa mikononi mwa ISIS katika nchi za Kiislamu katika miezi 7 ya kwanza mwaka huu.

Jones anasema ISIS haitetei maslahi ya misingi ya Uislamu pamoja na kuwa wengi wanalitazama kundi hilo la kigaidi kuwa linapigana kwa jina la Uislamu.

Aidha amebaini kuwa ISIS inatumia jina la Uislamu kama njia ya kufunika malengo yake ya kisiasa huku likiibua mgawanyiko baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu duniani. Mwanachuo huyo wa Scotland amelalamika kuwa kila mara kunapojiri hujuma ya kigaidi ya ISIS katika nchi isiyokuwa ya Waislamu, kunashuhudiwa chuki dhidi ya Waislamu na hilo ndilo jambo ambalo ISIS inalenga kufikia. Kwa kufanya hivyo ISIS inataka Waislamu wahisiwametengwa na hivyo iwe rahisi kuwaingiza katika kundi hilo la kigaidi. Jones anasema njia pekee ya kukabiliana na ISIS ni kutmabua kuwa kundi hilo halipigani kwa niaba ya Uislamu.

Katika taarifa, Toni Jones, mwanafunzi wa taaluma ya sheria katika Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland ameashiria hujuma za kigaidi katika Msikiti wa Mtume SAW, Al-Masjid an-Nabawi, mjini Madina mnamo Julai 4, na kabla ya hapo hujuma za kigaidi Baghdad, Dhaka na Istanbul na kusema hujuma hizo zote, ambazo ISIS ilidai kuhusika nazo, zimefanyika katika nchi za Kiislamu.  Amesema kuna dhana potovu kuwa ISIS ni kundi la kigaidilinalpigana kwa niaba ya Uislamu. Mwanachuo huyo wa Scotland amesema wengi hawafahamu kuwa, tokea kuibuka kwake, ISIS imewaua Waislamu wengi zaidi ya wasiokuwa Waislamu. Ameongeza kuwa, ukweli huu unapuuzwa na wengi wakati hujuma ya kigaidi inapojiri katika miji ya nchi za Magharibi.
Ameashiria ripoti ya mwaka 2009 ya Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha Westpoint ambayo  ilibaini kuwa watu waliouawa na kundi la al Qaeda, ( ambalo ni chimbuko la ISIS), kati ya mwaka 2004 na 2008 ni asilimia 12 tu waliokuwa raia wa nchi za Magharibi, jambo ambalo linamaanisha kuwa al Qaeda iliua Waislamu mara saba zaidi ya wasiokuwa Waislamu. 
Kuhusiana na ISIS ukweli ni huo huo. Katika mwaka 2016 pekee, ISIS imetekeleza hujuma za kigaidi 21 na 18 kati yazo zimetekelezwa katika nchi zenye Waislamu wengi hama vile Iraq, Syria, Saudi Arabia na Uturiki. Aidha watu waliouawa na ISIS katika nchi zisizo za Kiislamu hadi kufikia sasa katika mwaka 2016 ni 83 katika hali ambayo Waislamu zaidi ya 677 wameuawa mikononi mwa ISIS katika nchi za Kiislamu katika miezi 7 ya kwanza mwaka huu.
Jones anasema ISIS haitetei maslahi ya misingi ya Uislamu pamoja na kuwa wengi wanalitazama kundi hilo la kigaidi kuwa linapigana kwa jina la Uislamu.
Aidha amebaini kuwa ISIS inatumia jina la Uislamu kama njia ya kufunika malengo yake ya kisiasa huku likiibua mgawanyiko baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu duniani. Mwanachuo huyo wa Scotland  amelalamika kuwa kila mara kunapojiri hujuma ya kigaidi ya ISIS katika nchi isiyokuwa ya Waislamu, kunashuhudiwa chuki dhidi ya Waislamu na hilo ndilo jambo ambalo ISIS inalenga kufikia. Kwa kufanya hivyo ISIS inataka Waislamu wahisiwametengwa na hivyo iwe rahisi kuwaingiza katika kundi hilo la kigaidi. Jones anasema njia pekee ya kukabiliana na ISIS  ni kutambua kuwa kundi hilo halipigani kwa niaba ya Uislamu.
Kishikizo: isis waislamu ugaidi iqna
captcha