IQNA

Rais Rouhani wa Iran atuma salamu za Idi kwa Waislamu duniani

11:12 - September 12, 2016
Habari ID: 3470559
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia viongozi wa nchi za Kiislamu na Waislamu duniani salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa siku kuu ya Idul Adha.

Katika ujumbe wake huo, Rais Hassan Rouhani amewatumia viongozi hao na Waislamu wote salamu katika munasaba wa Idi hii kubwa.

Rais wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa: "Waislamu wataweza kunufaika na baraka za kimaanawi na kijamii za Idul Adha na hasa msimu wa Hija. Aidha amesema ana matumaini kuwa, kwa ushirikiano na maelewano zaidi, Waislamu wataweza kuwasilisha kwa dunia Uislamu halisi wa Bwana Mtume Muhammad SAW ambaye alikuwa msingi wa rahma na uadilifu.

Katika ujumbe huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Waislamu wanapaswa kuimarisha umoja wao na kuondoa mifarakano na chuki katika umma.

Rais Rouhani amewatakia Waislamu wote duniani mafanikio katika kuimarisha misingi ya udugu na mahaba. Leo tarehe 10 Dhilhaj ni sikukuu ya Idul Adha, moja ya sikukuu kubwa za Kiislamu.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, yaani Bunge la Iran, Ali Larijani naye pia amewatumia salamu za kheri na fanaka maspika wa mabunge ya nchi za Kiislamu kwa munasaba wa Siku Kuu ya Idul Adha. Katika ujumbe wake ambao pia amewatumia shakhsia wa Kiislamu, Larijani ametoa wito wa umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu. Huku akiashiria matatizo ya leo ya Umma wa Kiislamu hasa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina ikiwemo Quds Tukufu, na wimbi la fitina ya magaidi wakufurishaji, Larijani amesema kwa umoja Waislamu wanaweza kukabiliana na changamoto hizo.

3529597/

Redio Tehran inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa sikukuu hii kubwa.


captcha