IQNA

Mufti wa Saudia: Maulid ya Mtume SAW ni Shirki, sherehe za ukoo wa Aal Saud ni wajibu wa kidini!

19:02 - September 27, 2016
1
Habari ID: 3470582
Mufti katika kasri ya ufalme wa Saudia amesisistiza kuwa kusherehekea Maulid ya Mtume Muhammad SAW ni shirki lakini akasema ni wajibu kusherehekea maadhimisho ya kuanza kutawala ukoo wa Aal Saud.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Abdulaziz Aal Sheikh, Mufti Mkuu wa Saudia, sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad SAW ni sherehe zisizo na msingi wa kidini. Aidha amedai kuwa sherehe  hizo ni potofu na ni shirki huku akiwaonya wanaoshiriki katika Maulid ya Mtume Mtukufu SAW.

Lakini katika upande wa pili, sambamba na maadhimisho ya kunyakua madaraka ukoo wa Aal Saud katika ardhi ya Hijaz ambayo iliadilishwa jina na kuwa Saudi Arabia, Mufti huyo amegeuka daraja 180 na  kutoa fatwa mpya ya kuwalazimisha wananchi kusherehekehea siku hiyo. Sheikjh Abdul Aziz Aal Sheikh amebadilisha jina la Siku ya Kitaifa na kuitaja kuwa 'Siku ya Kushukuru' na kusema ni wajibu wa kidini kuisherehekea.

Maulamaa wa Kiwahhabi wanawakera Waislamu waliowengi kwa misimamo yao ya kufurutu adha ya kuharamisha Maulid ya Bwana Mtume SAW.

Magaidi wakufurishaji wanafuata itikadi za Kiwahhabi wamekuwa wakitekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wanaoshiriki katika Maulid ya Mtume SAW.

Mufti wa Saudia:Maulid ya Mtume SAW, sherehe za ukoo wa Aal Saud ni wajibu wa kidini!

3533546


Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
hiyo hoja ya mashia sio mtume akushereke kuzaliwa kwake wala uislam hauna ila kwa mashia ndio kwa
captcha