IQNA

Iran, Ghana kuimarisha uhusiano wa kidini

17:02 - November 02, 2016
Habari ID: 3470647
IQNA-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimiakuimarisha uhusiano wake wa kidini na Ghana.

Hayo yamebainika katika mkutano baina ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Ghana Mohammad Hassan Ipakchi na George Ossom-Batsa Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya Kidini katika Chuo Kikuu cha Ghana mapema wiki hii.

Katika kikao hicho, wawili hao walijadili njia za kuimarisha uhusiano wa kidini baina ya nchi mbili ambapo Bw. Ipakchi aliarifisha harakati za Shirika la Iran la Mahusiano ya Kiislamuna Utamaduni ICRO hasa katika uga wa mazungumzo baina ya dini. Amesema Irna inalipa umuhimu suala la ushirikiano na Ghana katika vikao vya mazungumzo baina ya dini.

Bw. Ipakchi aidha amepongeza namna wafuasi wa dini mbali mbali wanavyoishi kwa Amani na maelewano nchini Ghana.

Kwa upande wake Ossom-Batsa amesisitiza umuhimu wa Iran na Ghana kujihusisha na mazungumzo baina ya dini. Mwzi Machi kulikuwa na kikao cha mazungumzo ya kidini baina ya nchi mbili katika Chuo Kikuu cha Ghana, Legon. Uislamu ni moja ya dini muhimu nchini Ghana ambapo Waislamu ni zaidi ya asilimia 20 ya wato wote milioni 27 katika nchi hiyo huku Wakristo wakiwa asilimi 41.

captcha