IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu, chanzo cha kuhujumiwa misikiti Afrika Kusini

11:21 - January 14, 2017
Habari ID: 3470793
IQNA: Serikali ya Afrika Kusini imesema chuki dhidi ya Uislamu ndio chanzo cha hujumza mbili dhidi ya misikiti mjini Cape Town.
Chuki dhidi ya Uislamu, chanzo cha kuhujumiwa misikiti Afrika Kusini

Katika taarifa, serikali ya eneo la Cape Magharibi imeashiria matukio ya hivi karibuni ambapo damu ilipakwa katika kuta za msikiti Kalk Bay na hujuma nyingine ya msikiti wa Simon Town ambapo pua la nguruwe liliwekwa msikiti na kusem, "matukio hayo mawili ni njama ya makusudi ya chuki dhidi ya Uislamu." Taarifa hiyo imesema kwa kuzingatia kushabihiana vitendo hivyo viwili na kukaribiana misikiti iliyolengwa kuna wasi wasi kuwa vitendo hivyo viwili vinahusiana."

Sheikh Achma Sity, Imamu wa Msikiti wa Kalk Bay uliojengwa miaka 110 iliyopita ametoa wito wka Waislamu kuwa watulivu na kudumisha umoja.

"Msikiti huu umekuwepo hapa kwa zaidi ya miaka 100 na ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kujir," amemwambia mwandisi wa Al Jazeera.

Tawi la chama tawala cha ANC katika eneo hilo limelaani hujuma hiyo na kuoitaja kuwa ya "kuchukiza" sambamba na kutoa wito kwa watu wa Afrika Kusini kudumisha umoja na kulinda utamaduni wa kustahamiliana.

Farid Sayed, mhariri wa jarida la Muslim Views amesema hujuma hizo zinaashiria kuwa baadhi ya watu wameshindwa kujiunga na jamii nzima baada ya mfumo wa ubaguzi wa rangi kupinduliwa Afrika Kusini.

Amesema vyombo vya habari vya mrengo wa kulia vinachochea hisia za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Habari ya tukio hilo la chuki dhidi ya Uislamu ambalo lilitokea katika msikiti wa eneo la Simon Jumamosi iliyopita baada ya Sala ya Alfajiri ilienezwa kupitia mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, wakati polisi ya mji wa Simon ilipopewa taarifa ya tukio hilo ilieleza kwamba hakuna inachoweza kufanya na kwa hivyo haitofungua kesi kuhusiana na tukio hilo

Kati ya watu 55 milioni nchini Afrika Kusini asilimia 1.5 ni Waislamu na wengi wana nafasi muhimu za kisiasa, katika vyuo vikuu, biashara n.k

http://iqna.ir/en/news/3461926

captcha