IQNA

Wakuu wa vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu wakutana Ankara

23:12 - July 27, 2017
Habari ID: 3471091
TEHRAN (IQNA)-Wakuu wa vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu wamekutana Ankara, mji mkuu wa Uturuki na kujadili kuundwa Baraza Kuu la Kiislamu la Ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,mkutano huo uliofanyika Julai 26-27 uliandaliwa na Jukwaa la Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu (FUIW) kwa ushirikiano wa Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) pamoja na Baraza Kuu la Elimu Uturuki.

Mkutano huo ulifunguliwa kwa hotuba ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ambaye alisema kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua hatua kuzuia wasomi Waislamu kukimbilia katika nchi za Magharibi. Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa kati ya vyuo vikuu 500 bora duniani, vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu ni vichache mno. Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa katika hali ambayo aghalabu ya nchi za Ulaya hutenga asimilia 5.2 ya bajeti ya kitaifa kwa ajili ya elimu, katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla ni asilimia moja tu.

Washiriki wa mkutano wa Ankara wamejadili njia za kuimarisha ushirikiano baina ya vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu katika nchi za Kiislamu.

3623282

captcha