IQNA

Saudia inaunga mkono mauaji ya Waislamu Mashia nchini Nigeria

13:51 - April 27, 2018
Habari ID: 3471484
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky ameituhumu Saudi Arabia kuwa inaliunga mkono kifedha Jeshi la Nigeria ili litekeleza mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Zakzaky ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na mwanae ambapo pia amebainisha upinzani wake kwa masharti ambayo serikali imetoa ili aachiliwe huru. Sheikh Zazaky amebaini kuwa: "Saudi Arabia, kwa amri ya Marekani na Uingereza, inaliunga mkono Jeshi la Nigeria ambalo limetekeleza mauaji dhiid ya Mashia wa mjini Zaria."

Sheikh Zakzaky  aidha amesisitiza kuwa ataendelea na msimamo wake ambao amekuwa nao na wala hatalegeza msimamo.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka.

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo.

3709521

captcha