IQNA

11:32 - August 25, 2018
1
News ID: 3471645
TEHRAN (IQNA)- Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Matiafa UNICEF umelaani vikali hujuma ya hivi karibuni ya ndege za kivita za Saudia katika mkoa wa Hudaydha ambapo watoto 26 waliuawa.

Siku ya Alkhamisi ndege za kivita za Saudi Arabia zilidondoshea mabomu magari mawili ya wakimbizi Wayemen katika eneo la Ad Durayhimi katika mkoa wa al Hudaydah magharibi mwa Yemen ambapo watu 31 wakiwemo watoto 26  na wanawake waliuawa.

Jinai hiyo imejiri takribani wiki mbili tu baada ya ndege za kivita za utawala wa Saudia zilifanya shambulizi jingine la kinyama dhidi ya basi lililokuwa limewabeba wanafunzi wa Qur'an Tukufu shambulizi lililofanyika eneo la Dhahiyan la mkoa wa Saada, ambapo kutokana na hujuma hiyo watoto 55 waliuawa na wengine 77 walijeruhiwa.

Katika taarifa, mkurugenzi wa UNICEF Henrietta Fore amesema ilitarajiwa baada ya hujuma hiyo ya Sa'ada kulaaniwa Saudia ingechukua tahadahri zaidi lakini hujuma ya Ad Durayhimi na kuuawa watoto 26 ni jambo linanaloashiria haikuwa ilivyotarajiwa. Ametoa wito kwa Baraza la Usalama na jamii ya kimatiafa kuchukua hatua za kumaliza hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen huku akisisitiza kuwa maelefu ya watoto waliohatarini katika vita vya Yemen wanapaswa kupewa kipaumbele.

Jinai za utawala wa Saudia dhidi ya raia wa Yemen zinafanyika mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani jinai mpya za ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia nchini Yemen ambazo zimelenga wanawake watoto wakimbizi nchini Yemen. Msemaji wa WIzara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bahram Qassemi katika ujumbe aliotoa jana Ijumaa, sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za waathirika wa jinai hiyo amesema: "Ikiwa bado haijapita muda mrefu tokea ndege za kivita za Saudia zidondoshee bomu basi lililokuwa limebeba watoto wa shule katika mji wa Dahyan mkoani Saada ambapo zaidi ya watoto 130 waliuawa na kujerhiwa, dunia imeshuhudia jinai nyingine dhidi ya watu madhulumu wa Yemen.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia.

3466595

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
Abuuraahim
0
0
Dunia inaitaji amani sio kuuana
Name:
Email:
* Comment: