IQNA

16:09 - September 01, 2018
News ID: 3471655
TEHRAN (IQNA)- Mahakama ya Afrika Kusini imeamuru ndoa za Kiislamu zitambuliwe na serikali ili kuwalinda wanawake wakati wa talaka.

Katika hukumu iliyotolewa Ijumaa, Mahakama Kuu ya Cape Magharibi imeamuru, 'kutungwe sheria za kutambua ndoa ambazo zimefungwa kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu kuwa ni ndoa zinazotambulika rasmi."

Kwa mujibu wa sheria za sasa, ndoa za Kiislamu hazitambuliwi kisheria na hivyo kuibua changamoto wakati wa talaka.

Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya Kituo cha Sheria cha Wanawake (WLC) kuwasilisha lalamiko kuwa wanawake walio katika ndoa za Kiislamu hawapati kinga ya kisheria hasa wakati wa talaka.

WLC imesema kuwa wanawake Waislamu walio katika ndoa za Kiislamu huwa hawapati haki zao wakati wa talaka.

Wakati huo huo Baraza la Kisheria la Waisalmu Afrika Kusini (MJC) limepongeza uamuzi huo wa mahakama ambao ulitolewa na Jaji Siraj Desai. "Ni hatua muhimu kwa Waislamu ambao ni jamii ya waliowachache Afrika Kusini," amesema naibu mwenyekiti wa MJC Sheikh Riad Fataar. Aidha ametoa wito kwa Rais Cyril Ramaphosa kuweka historia kwa kutambua ndoa za Waislamu.

Waislamu nchini Afrika Kusini wanakadiriwa kuwa ni asilimia 2 ya watu wote milioni 55 nchini humo.

3466663/

Name:
Email:
* Comment: