IQNA

11:58 - January 26, 2019
News ID: 3471819
TEHRAN (IQNA)-Fainali ya Mashindano ya 22 ya Qur'ani ya Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yameanza mjini humo Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ya Qur'ani yanajumuisha washiriki 1,000 kutoka maeneo mbali ya UAE.

Aidha raia wa kigeni ambao wanaishi nchini humo wanaruhusiwa kushiriki katika mashindano.

Kila mwaka Mashindano ya Qur'ani ya Sharjah huandaliwa na Taasisi ya Qur'ani na Sunnah ya Sharjah na huwa na vitengo viwili vya wanawake na wanaume. Washiriki hushindana katika kuhifadhi Qur'ani na Hadithi za Mtume Muhammad SAW. Mchujo wa mashindano hayo ulifanyika mwezi uliopita.

3784224

Name:
Email:
* Comment: