IQNA

14:51 - February 02, 2019
News ID: 3471827
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iliyoko nchini Iraq imezindua Taasisi ya Qur'ani nchini Burkina Faso.

Taasisi ya Warith al Anbia imefunguliwa katika mji wa Bobo Dioulasso , ambao ni mji mkuu wa pili kwa ukubwa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Taasisi hiyo ni tawi la Taasisi ya Warith al-Anbia iliyo Karbala nchini Iraq na inajihusisha na utoaji mafunzi kwa waalimu wa Qur'ani na wahubiri wa Kiislamu. Ujumbe wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS umetembelea Burkina Faso kwa lengo la kuhshiriki katika uzinduzi wa taasisi hiyo,

Burkina Faso ni nchi iliyo Afrika Magharibi na imezungukwa na Mali upande wa kaskazini, Nigeria upande wa Mashariki, Benin upande wa kusini mashariki, Togo na Ghana upande wa kusini na Kodivaa upande wa kusini magharibi.

Uislamu una historia ndefu sana nchini Burkina Faso ambapo kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2010, karibu asilimia 62 ya wakazi watoe wa nchi hiyo ni Waislamu.

Taasisi ya Qur'ani kuzinduliwa Burkina Faso

Taasisi ya Qur'ani kuzinduliwa Burkina Faso

Taasisi ya Qur'ani kuzinduliwa Burkina Faso

 

3786314

Name:
Email:
* Comment: