IQNA

Moja ya mashirika ya matangazo ya kibiashara nchini India, katika kipindi hiki cha kukaribia mwaka mpya wa Nairuzi nchini humo, limetengeneza filamu fupi ya tangazo la kibiashara yenye lengo la kuhimiza mshikamano wa wafuasi wa dini zote katika sherehe hii ya kila mwaka.

Katika filamu hii,  binti mmoja anakubli apigwe kwa rangi za Holi ili amlinde rafiki yake ambaye ni Mwislamu aliyekuwa anaenda msikitini asichafuliwe kwa rangi hizo.

Tamasha la Holi ni kati ya sherehe rasmi za na za kitaifa na kidini India katika msimu wa machipuo ambayo huwashirikisha wananchi wa India hasa Wahindu au Mabaniani.