IQNA

Mesut Ozil atoa msaada wa futari kwa Waislamu Somalia, Uturuki na Syria

22:34 - May 03, 2020
Habari ID: 3472730
TEHRAN (IQNA) – Mesut Ozil mchezaji soka mashuhuri wa timu ya Arsenal katika Ligi ya Premier ya England ametoa mchango wa dola laki moja za Kimarekani kuwasaidia Waislamu ambao wameathiriwa vibaya na janga la COVID-19 au corona katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa, msaada wa Ozil, ametoa mchango huo ambao utatumika kununua futari kwa ajili ya watu 16,000 nchini Uturuki na Syria katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha fedha hizo pia zitatumika kununua vifurishi 90,000 vya futari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu ya Uturuki Kerem Kinin amemshukuru mchezaji soka huyo na amemhakikishia kuwa misaada hiyo itawafikia wanaohitaji haraka iwezekanavyo.

Ozil, ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki, ni kati ya wachezaji wanaolipwa kitita kikubwa zaidi katika timu ya Arsenal. Ozil ni Mwislamu anayefungamana na mafundisho ya Kiislamu na  huwasaidia maelefu ya watoto wanaohitaji matababu huku akitoa msaada wa chakula kwa makumi ya maelfu ya familia kila mwaka.

3471341

captcha