IQNA

Maandamano ya kuunga mkono Palestina yafanyika Scotland

17:37 - September 05, 2020
Habari ID: 3473140
TEHRAN (IQNA) - Wanaharakati wanaounga mkono Palestina wameandamana nje ya uwanja wa mpira wa Hampden Park, huko Glasgow, Scotland nchini Uingereza kulaani mechi iliyochezwa Ijumaa katika ya timu ya taifa ya Scotland na kalbu moja ya soka ya utawala bandia wa Israel.

Maandamano hayo ambayo yaliandaliwa na ‘Kampeni ya Mshikamano wa Palestina na Scotland’ ilifanyika pia kulaani jinai za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na uporaji wa ardhi zaidi za Palestina unaofanywa na utawala huo ghasibu.

Waandamanaji wanasema wameaibishwa na kitendo cha Shirikisho la Soka Scotland kualika timu hiyo ya Israel. Mapmea wachezaji soka Wapalestina walikuwa wametoa wito wa kususiwa mechi hiyo kutokana na ugaidi unaotendwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wanamichezo Wapalestina.

3472466

captcha