IQNA

Uislamu na Ukristo

Rais wa Iran amtumia Papa Francis Salamu za Krismasi

16:39 - December 26, 2022
Habari ID: 3476309
TEHRAN (IQNA)- Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za pongezi kwa mnasaba wa siku ya kuzaliwa Nabii Isa bin Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-na kuwadia mwaka mpya wa Miladia.

Katika ujumbe kwa Papa Francis, kiongozi wa Wakatoliki duniani, rais huyo amempongeza pamoja na wafuasi wote wa Ukristo kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabii Isa (Yesu) na kuwadia mwaka mpya wa 2023.

Seyyed Ebrahim Raisi, katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa kiongozi wa Wakatoliki duniani, huku akirejelea aya za Qur'ani Tukufu katika Surah Maryam kuhusu nafasi adhimu ya Nabii Isa Masihi katika Qur'ani Tukufu na maneno yake kuhusu huruma, uhuru wa kweli, bishara ya mwokozi na wokovu wa wanadamu.

Rais wa Iran ameelezea matumaini kwamba katika mwaka mpya, kwa msaada wa mafundisho ya thamani ya Mitume wa Mwenyezi Mungu akiwemo Isa bin Maryam (AS) na kudumu katika njia ya maadili ya Mwenyezi Mungu, furaha ya mwanadamu itapatikana na ulimwengu uliojaa haki na huruma utaundwa miongoni mwa mataifa.

Wakatoliki na Waprotestanti huadhimisha Krismasi Disemba 25, huku Waothodoksi wakiadhimisha kumbukumbu ya mazazi hayo ya Nabii wa Allah, Isa Masih (AS) Januari 7.

Isa Masih (AS) ni mmoja wa Mitume wakubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye ametajwa kwa heshima na taadhima kubwa katika Qur'ani Tukufu, na inamtambulisha kama mmoja wa Manabii wakuu waliopewa Kitabu na sheria na Mwenyezi Mungu.

4109677

captcha