IQNA

Siasa za Saudia

Mhubiri maarufu Saudi Arabia ahukumiwa kunyongwa

21:07 - January 15, 2023
Habari ID: 3476408
TEHRAN (IQNA)- Taarifa zinasema mhubiri mmoja mashuhuri nchini Saudi Arabia amehukumiwa kunyongwa katika kile kinachoongokana ni ukandamizaji dhidi ya wanaopinga sera za Ufalme huo.

Mhubiri na msomi wa Saudia mwenye umri wa miaka 66, Awad bin Mohammed Al-Qarni, amehukumiwa kifo kwa kutumia mitandao ya kijamii - Twitter, Facebook, WhatsApp na Telegram, kueneza habari zinazochukuliwa kuwa "uhasama" kwa Ufalme.

Gazeti la Guardian la Uingereza limedai kuwa limeona nyaraka za mahakama ya Saudia na maelezo ya kina ya mashtaka dhidi ya Al-Qarni na mwanawe, Nasser, ambaye alitoroka Ufalme wa Saudia mwaka 2022 na kwa sasa anaishi Uingereza baada ya kuomba hifadhi.

Mashtaka dhidi ya Al-Qarni, ni pamoja na kukiri kwamba alitumia akaunti ya Twitter chini ya jina lake (@awadalqarni) na kuitumia "katika kila fursa ... kutoa maoni yake."

Nyaraka za mahakama pia zinaonyesha kwamba "alikiri" kushiriki katika mazungumzo ya WhatsApp, na alishtakiwa kwa kushiriki katika video za kusifu Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri.

Gazeti hilo limemnukuu Jed Bassiouni, Mkuu wa Mawakili wa Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika katika shirika la kutetea haki za binadamu la “Reprieve akisema: “Kesi ya Awad Al-Qarni iko katika hali ambayo mahakama ya Saudi Arabia imetoa hukumu za kifo na kifungo kwa baadhi ya watu wakiwemo wahubiri na wakosoaji kwa uchapisha taarifa katika twitter.

Awad Al-Qarni ni mhubiri na msomi maarufu  wa Saudi ambaye aliwahi kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Imam Muhammad bin Saud na Chuo Kikuu cha Mfalme Khalid. Ameandika vitabu kuhusu kuhusu fiqhi ya Kiislamu na suala la Palestina.

Al-Qarni aliwasilisha taarifa pamoja na maulama wengine 25 wakilaani uvamizi wa Iraq mwaka 2003 na taarifa nyingine inayoonyesha mshikamano na Wapalestina.

Aidha amewahi kukosoa sera Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman ambaye anatekeleza sera zenye lengo kuleta mabadiliko ya kisiaasa na masuala ya burudani, na kwa msingi huo Al-Qarni amehukumiwa kunyongwa kutokana na kuwa misimamo yake inakinzani na ile ya Mohammad bin Salman  ambaye kimsingi ndie mtawala wa Saudia.

4114857

captcha