IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Kenya apongeza Mashindano ya Qur'ani ya Iran

18:47 - February 22, 2023
Habari ID: 3476604
TEHRAN (IQNA) Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Kenya ambaye ameshika nafasi ya pili katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika fainali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran amepongeza kiwango cha mashindano hayo na kusema ni ya aina yake duniani.
Ustadh Abdulhalim Abdulrahim katika mahojiano na IQNA, pia ametoa wito kwa vijana wa Kiislamu kujitahidi katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Hapa chini ni mahojiano yake na IQNA.
 

Duru hii ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ilifanyika katika hatua mbili, ambapo duru ya kwanza ilifanyika kwa njia ya intaneti miezi kadhaa iliyopita na kushirikisha wagombea 150 kutoka nchi 80.

Kutoka miongoni mwao, maqari wa Qur'ani na waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 33 walifika kwenye fainali iliyofanyika mjini Tehran Februari 18-22. Mashindano hayo yalifunguliwa sambamba na mnasaba wa kukumbuka Kubaathiwa au kupewa utume, Mtume Muhammad SAW.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu, kama lile lililotangulia, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu mkubwa umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali.

captcha