IQNA

Mwezi wa Ramadhani

UAE yapunguza masaa ya kufanya wakati wa Mwezi wa Ramadhani

21:02 - March 14, 2023
Habari ID: 3476702
TEHRAN (IQNA) – Saa za kazi kwa wafanyakazi wa sekta binafsi zitapunguzwa kwa saa mbili wakati wa Mwezi Mtukufu Ramadhani katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Wizara ya Rasilimali Watu ya UAE imetangaza Jumatatu kwamba kampuni zitaweza kuanzisha "mifumo rahisi au kufanya kazi nyumbani" katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Saa za kandarasi hutofautiana katika sekta ya kibinafsi, na wafanyikazi wengi hufanya kazi kwa masaa tisa kila siku.

"Kulingana na mahitaji na asili ya kazi zao, kampuni zinaweza kutumia mifumo ya kufanya kazi inayoweza kubadilika au kufanya kazi nyumbai katika mipaka ya saa za kazi za kila siku wakati wa siku za Ramadhani," wizara ilisema.

UAE ilithibitisha saa za kazi kwa wafanyikazi wa serikali ya shirikisho wakati wa Ramadhani siku ya Ijumaa.

Mamlaka ya Idara ya Wafanyakazi wa Serikali ilisema katika waraka kwamba siku ya kazi itaanza saa tatu asubuhi hadi nane unusu mchana kutoka Jumatatu hadi Alhamisi, na kutoka tatu asubuhi hadi saa sita mchana Ijumaa.

Wizara na idara za shirikisho zitaruhusiwa kutekeleza ratiba za kazi zinazobadilika au kufanya kazi nyumbani.

Mwaka huu, Ramadhani inatarajiwa kuanza katika UAE Machi 23, lakini tarehe kamili huenda ikatangazwa usiku wa Machi 22 na kamati ya kuona mwezi.

3482796

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uae ramadhani
captcha