IQNA

Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) walaani kuvunjiwa Heshima Qur'ani Tukufu

13:59 - June 25, 2023
Habari ID: 3477191
Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umelaani kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu na waenezaji wa Kizayuni, na kueleza kuwa ni ukatili na fedheha.

Muungano huo siku ya Ijumaa umelaani vikali  kutekwa kwa kitabu kitakatifu cha Waislamu na walowezi wa Israel ambao waliharibu msikiti katika mji wa Urif katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Kitendo hiki cha kinyama na cha aibu kilikuwa shambulio la wazi dhidi ya maadili matukufu  ya Uislamu na kililenga hisia za Waislamu wote ulimwenguni, ulisema umoja huo wenye makao yake mjini Doha.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki pia ililaani kisa hicho siku ya Alhamisi na kuelezea wasiwasi wake kuhusiana na mvutano uliozuka katika eneo hilo katika siku za hivi karibuni.

Tunalaani shambulio lililofanywa na kundi la walowezi wa Kiyahudi kwenye kitabu chetu kitukufu, cha Quran Tukufu  kwa kuingia katika msikiti katika mji wa Urif, ulioko katika ardhi za Palestina chini ya utawala wa Israel ilisema.

Mvutano umekuwa ukitanda katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu katika miezi ya hivi karibuni huku kukiwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel katika miji ya Palestina.

Takriban Wapalestina 180 wameuawa na wanajeshi wa Israel tangu kuanza kwa mwka  2023, kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina, Takriban Waisrael 25 pia wameuawa katika mashambulizi tofauti katika kipindi hicho.

Makadirio yanaonyesha walowezi 700,000 wanaishi katika makazi 164 na vituo 116 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Chini ya sheria za kimataifa, makazi yote ya Wayahudi katika maeneo yanayokaliwa yanachukuliwa kuwa haramu.

 

 

3484059



Kishikizo: jinai za israel qurani
captcha