IQNA

Suluhisho la Qur'ani kwa matatizo ya Familia/1

Mlingano na Kafa’ah katika Ndoa

22:04 - November 07, 2023
Habari ID: 3477858
TEHRAN (IQNA) – Tatizo la kukosekana kwa usawa katika kiwango cha elimu, mali, n.k, kati ya mwanamume na mwanamke wanaooana linaweza kusababisha migogoro na wanandoa wanaweza kuishia kwenye talaka kutokana na hilo.

Hapa tunajadili mtazamo wa Qur'ani Tukufu juu ya suala hili.

Kafa’ah ni miongoni mwa mahitaji muhimu sana katika ndoa na jambo kuu katika nguvu na uimara wa familia.

Kafa’ah ni neno linalotumika katika uwanja wa sheria za Kiislamu kuhusiana na ndoa katika Uislamu, ambalo kwa Kiarabu, maana yake halisi ni, usawa au mlingano. Kwa hivyo inafafanuliwa kama mlingano au usawa kati ya mume mtarajiwa na mke wake mtarajiwa ambao unapaswa kuzingatiwa. Mlingano huu unategemea mambo mengi ambayo ni pamoja na dini, hadhi ya kijamii, umri, maadili, uchamungu, utajiri, ukoo au desturi.

Uzoefu unaonyesha kwamba pamoja na nyanja za kiroho na kimaadili, panapaswa kuwepo Kafa’ah kati ya mume na mke katika suala la mali pia.

Katika Qur'ani Tukufu, sababu nyingi zimetajwa za ulazima wa Kafa’ah kati ya mume na mke. Hapa kuna mmoja wao:

"Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.” (Aya ya 221 ya Surah Al-Baqarah)

Wanachuoni wa madhehebu ya Shia na Sunni wanaamini kwamba kwa kuzingatia aya hii, kuoa mwanamume Mwislamu na mwanamke mpagani na kuoa mwanamke wa Kiislamu na mwanamume mpagani hairuhusiwi.

Hivyo Muumini, awe mwanamume au mwanamke, aolewe na Muumini. Hata kama mtu ana matatizo ya kifedha na hawezi kuolewa na Muumini, haruhusiwi kuolewa na kafiri kwa sababu itadhoofisha imani yake na maisha yake ya kiroho hapa duniani na matatizo ya kesho akhera. Pia, tofauti za imani huibua mvutano na taharuki katika familia.

Kwa hivyo, mtu anapaswa kuzingatia sana kuchagua mume au mke ili kuwe na Kafa’ah na mlingano katika suala la imani, vitendo na tabia.

Hili lapasa kutiliwa maanani na mwanamume na mwanamke pamoja na wazazi wao na watu wa ukoo ambao wana jukumu la kuwachagulia mwenzi.

Kishikizo: Ndoa
captcha