IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Qur’ani Tukufu ya Jeshi la IRGC la Iran yaaanza

21:57 - December 21, 2023
Habari ID: 3478071
IQNA - Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 42 Qur'ani Tukufu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) yamezinduliwa katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran siku ya Alhamisi.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Hossein Salami alihutubia kwenye hafla ya ufunguzi, akielezea IRCG kama jeshi ambalo ni dhihrisho la aya nyingi za Qur’ani Tukufu katika dunia ya leo

Amesema Qur'ani Tukufu inawaalika wote, wakiwemo wanajeshi wa IRGC, kufanyia kazi mafundisho yake.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa IRGC wanapaswa kuakisi aya za Qur'ani Tukufu katika mwenendo wao.

IRGC inataka kukuza imani, itikadi na utamaduni wa Kiislamu duniani, aliendelea kusema.

Kwingineko katika matamshi yake, Meja Jenerali Salami ameashiria vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza na kusema Wazayuni watashindwa kwa fadhila zake Mwenyezi Mungu.

Akirejelea aya za Surah Al-Hashr za Qur'ani Tukufu, Majaor Jenerali Salami alisema hofu imetanda katika nyoyo za Wazayuni, ambao viongozi wao hawana busara.

Zaidi ya maafisa 10,000 walishiriki katika hatua ya awali ya mashindano hayo ya Qur’ani Tukufu ambapo  287 kati yao wamefuzu kwa raundi ya mwisho. Mashindano hayo yataendelea hadi Jumamosi, Desemba 23.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC au SEPAH)  lilianzishwa Aprili 22 1979 kufuatia amri ya Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kukabiliana na njama za maadui waliotaka kuvuruga mapindui ya Kiisalmu na kuulinda usalama wa Iran.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC au Sepah) ni chombo ambacho kimetokana na Mapinduzi ya Kiislamu na limeweza kuonyesha nguvu za taifa la Iran mbele ya maadui.

Katika zama za vita vya kulazimishwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilisimama bega kwa bega na majeshi mengine ya Iran katika kukabiliana na adui na lilionyesha ushujaa, moyo wa kimapinduzi na kuwa tayari kufa shahidi. Aidha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limeweza kupata mafanikio makubwa katika mstari wa mbele wa kupambana na makundi ya magaidi wakufurishaji nchini Iraq na Syria hasa kundi la kigaidi la ISIS na makundi mengine kama hayo.

4189207

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jeshi qurani tukufu irgc
captcha