IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Televisheni ya Al-Thaqalayn yazindua Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

20:38 - March 17, 2024
Habari ID: 3478531
IQNA - Televisheni ya satelaiti ya Al-Thaqalayn imeanza kurusha mashindano yake ya kwanza la kimataifa la usomaji wa Tarteel wa Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la  "Wa Rattil" (…na usome Qur'an kwa sauti tofauti- Aya ya 4 ya Surah Al-Muzzammil), ni mashindano ya Qur'ani yanayofanyika kwa njia ya televisheni hurushwa hewani kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Televisheni ya Al-Thaqalayn.

Qarii maarufu wa Qur'ani,  Ahmad Najafi ndiye mtayarishaji mashindano ya Qur'ani.

Mamia ya maqari kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu wamewasilisha faili za usomaji wao wa Qur'ani kwa mtandao wa TV, ambapo 100 kati yao wamefika kwenye duru kuu baada ya kupata pointi nyingi zaidi.

Kwa mujibu wa ofisi ya uhusiano wa umma ya Televisheni ya Al-Thaqalayn, wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi tofauti za Kiislamu wamealikwa kutathmini utendakazi wa wanaoshiriki.

Katika siku nane za kwanza, Ahmed Jassim al-Najafi kutoka Iraq, Ahmed Abdul Hakim kutoka Misri, Jalal Masoumi kutoka Afghanistan, na Mohammad Ali Dehdashti kutoka Iran wanahudumu katika jopo la majaji.

Tarteel ni neno la Kiarabu ambalo kwa kawaida humaanisha usomaji wa Qur'an "kwa mpangilio sahihi" na "bila haraka". Ni usomaji wa Qur'ani kwa sauti zenye mahadhi kwa mujibu wa kanuni zinazoeleza jinsi ya kusoma Quran.

Al-Thaqalayn ni kituo cha televisheni cha satelaiti kinachotangaza vipindi mbalimbali vyenye mada za kidini na kitamaduni.

Televisheni hiyo ya lugha ya Kiarabu, ambayo ilizinduliwa mwezi wa Ramadhani mwaka 2008, inalenga kukuza utamaduni wa Kiislamu na mafundisho ya Qur'ani Tukufu, Mtume Muhammad (SAW) na Ahl-ul-Bayt (AS).

Pia inalenga kuimarisha taasisi ya familia ya Kiislamu kupitia programu maalum za wanawake, watoto na vijana.

3487598

Habari zinazohusiana
captcha