iqna

IQNA

ayatullah khamenei
Idul Fitr
IQNA - Makumi ya maelfu ya waumini leo Jumatano asubuhi walikusanyika kwenye Uwanja  wa Swala wa Mosalla Imam Khomeini katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kwa ajili ya  Sala ya Idul Fitr inayoashiria kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3478667    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Kadhia ya Gaza
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Ghaza ni suala ambalo haliwezi kufumbiwa macho kwani ndiyo kadhia kuu ya Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, hivyo kila mmoja wetu anapaswa kutekeleza vizuri majukumu yake kuhusu Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3478666    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Sikukuu ya Idul Fitr
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anasema utawala wa Kizayuni wa Israel "lazima uadhibiwe na kutiwa adabu" kwa shambulio lake baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478662    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Siku ya Quds
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema siku ya Quds mwaka huu itakuwa uasi wa kimataifa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na kuongeza kuwa: "Utawala wa Kizayuni wa Israel utazabwa kibao usoni kutokana na shambulio lake dhidi ya majengo ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, mapema wiki hii."
Habari ID: 3478630    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/04

Jinai za Israel
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Majenerali walioongoka wa Kiislamu katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kusisitiza kwamba: "Taifa la Iran litawafanya Wazayuni wajutie jinai hiyo na jinai zingine kama hiyo."
Habari ID: 3478616    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/02

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema vikosi vya mapambano ya Kiislamu ya wapigania ukombozi au Muqawama na Wapalestina wote katika Ukanda wa Gaza ndio washindi kwenye medani ya vita na utawala wa Kizayuni wa Israel ni mwangamizaji wa kizazi na akasisitiza kwa kusema: kilele cha kuheshimika na kusimama imara watu wa Gaza na Palestina na kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita hivyo vya miezi sita ni tukio na jambo lenye rehma za Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3478598    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/29

Diplomasia ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, Muqawama (mapambano ya Kiislamu) usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu.
Habari ID: 3478588    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/27

Katika Ujumbe wa Mwaka Mpya wa 1403 Hijria Shamsia
IQNA-Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe muhimu kwa mnasaba wa Nowruz ambayo ni siku ya kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa 1403 Hijria Shamsia na ameuita mwaka huo kuwa ni wa kuongezeka kwa uzalishaji wa kiuchumi kwa kushirikisha wananchi.
Habari ID: 3478549    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/20

Ramadhani 1445 H
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislam mnamo Machi 13, siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1445 H, kama ilivyo ada kila mwaka wakati huu, alishiriki kwenye mahfali ya kushikamana na kuwa karibu na Qur'ani Tukufu iliyofanyika jijini Tehran. Hizi hapa ni picha za tukio hilo lililojaa nuru.
Habari ID: 3478507    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/14

Qur'ani katika Mwezi wa Ramadhani
IQNA- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, usomaji wa Qur'ani ni sanaa takatifu na inabidi lengo lake kuu liwe ni kuwafundisha watu na jamii maana na ujumbe uliomo kwenye Qur'ani na kuandaa mazingira ya kuzingatiwa aya za Kitabu hicho Kitakatifu kama ambavyo pia kilele cha istiqama ya wananchi wa Gaza kinatokana na kuielewa na kuifanyia kazi Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3478499    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/13

Siasa
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Iran ya Kiislamu haina ugomvi wowote na nchi, serikali na mataifa, bali inapinga dhulma na uchokozi uliomo ndani ya kambi ya demokrasia ya Magharibi.
Habari ID: 3478467    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/07

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepanda mzeituni katika hatua ambayo ameitaja kuwa ni mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Habari ID: 3478453    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/05

Uchaguzi wa Iran
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Maadui wa Iran ya Kiislamu wana hofu ya kushiriki kwa wingi kwa wananchi katika uchaguzi hapa nchini.
Habari ID: 3478428    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/28

Ulimwengu wa Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza kuhusu tukio chungu na la kuhuzunisha la Gaza na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni, na akasema: “masaibu ya Gaza ni masaibu ya wanadamu na yanaonyesha kuwa utaratibu wa sasa wa ulimwengu ni wa batili tupu, usioweza kudumu na utatoweka tu.
Habari ID: 3478321    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/08

Ulimwengu wa Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, anasema wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu wanabeba dhima nzito kuhusiana na matukio yanayojiri huko Gaza na kwamba wanapaswa kuanzisha matakwa ya umma ya kukata uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478310    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/05

Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amezuru Haram tukufu ya Imam Khomeini (MA) na makaburi ya Mashahidi ya Behesht Zahraa sambamba na kuanza maadhimisho ya Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3478280    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/31

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala wa Kizayuni kwa kukata mishipa muhimu ya uhai ya utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3478242    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/23

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika kikao cha maimamu wa Ijumaa kote Iran kuwa: Watu madhulumu na wenye nguvu wa Ghaza wameweza kuwaathiri walimwengu kwa mapambano yao.
Habari ID: 3478205    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/16

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama kubwa za maadui ni kuwatoa uwanjani wananchi wa Iran na kwamba Ukanda wa Gaza hivi sasa ni mfano wa wazi na wa kivitendo wa nguvu kubwa za wananchi huku akisisitiza kuwa historia haitasahau jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wanawake na watoto Wapalestina.
Habari ID: 3478174    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/09

Kadhia ya Palestina.
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema mpaka wa ulimwengu wa Kiislamu uko Gaza hivi leo, na kwamba Wapalestina wa eneo hilo wamesimama dhidi ya kiburi au mfumo wa kiistikbari na Marekani.
Habari ID: 3478140    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/03