Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi Mwakilishi wa Faqihi Mtawala
na Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran. Akizungumza na waandishi habari
Jumatatu mjini Tehran, amesema kutakuwa na washiriki 130 kutoka nchi 75
katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.
Amesema kwa mara ya kwanza mashindano yatafanyika
katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini MA, ili kuwezesha idadi
kubwa ya wananchi kujumuika katika mashindano hayo.
Sheikh Mohammadi ameongeza kuwa, mashindano ya mwaka huu yatakuwa na
washiriki kutoka mabara ya Afrika, Asia, Ulaya, Marekani na Oceania.
Ameongeza
kuwa mashindano hayo yatakuwa na
washiriki 57 katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na wengine 57
katika kategoria ya qiraa. Aidha amesema mwaka huu kutakuwa kitengo maalumu cha washiriki 16 wenye
ulemavu wa macho.
Sheikh
Mohammadi amebaini kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa na majaji 10 wa kigeni
na 8 kutoka Iran.
Aidha amesema washiriki wa mashindano hayo watapata pia fursa ya kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yataanza Jumatano wiki hii kuanzaia tarehe 11 hadi 17 Mei.
Rais Hassan Rouhani wa Iran anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya mwaka huu.
3496012