IQNA

Imamu wa Masunni Iran asema Saudia kuzuia Mahujaji Wairani si kwa maslahi ya Umma

12:32 - May 23, 2016
Habari ID: 3470330
Molawi Abdul Hamid Ismail Zehi, Imamu wa Msikiti wa Masunii wa Makki mjini Zahedan kusini mashariki mwa Iran amesema hatua ya Saudia kuwazuia Mahujaji Wairani mwaka huu si kwa maslahi ya Umma wa Waislamu.
Katika barua aliyomuandikia Mfalme Salman wa Saudi Arabia, Molawi Ismail Zehi ametoa wito wa kuandaliwa mazingira ya Wairani kushiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu.

Aidha ametoa wito wa kurejeshwa uhusiano wa kawaida baina ya Saudi Arabia na Iran na balozi za nchi mbili kufunguliwa ili Mahujaji Wairani waweze kushiriki ibada ya Hija bila vizingiti.

"Katika hali ya hivi sasa ambapo maadui wa Uislamu wanalenga kuibua mifarakano, migawanyiko na ukosefu wa matumaini miongoni mwa Waislamu duniani, kutoshiriki Mahujaji Wairani si kwa maslahi ya Ummah wa Kiislamu."

Molawi Ismali Zehi ameongeza kuwa Iran na Saudi Arabia ni nchi mbili muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu na zinaweza kuwa na nafasi kubwa katika kutatua matatiz mengi ya Ulimwengu wa Kiislamu.

Barua hiyo imekuja siku chache baada ya Iran kusema yamkini isiweze kutuma Mahujaji katika ibada ya Hija mwaka huu baada ya Saudia kukataa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuwawezesha Wairani kuelekea katika ibada hiyo ya kila mwaka mwezi Septemba.

Siku kadhaa zilizpopita, Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran Ali Jannati amesema, viongozi wa Saudi Arabia wanaendelea kukwamisha juhudi za Waislamu wa Iran za kwenda kutekeleza amali ya Hija mwaka huu.

Akizungumza Mei 12, alisematakriban miezi minne imepita sasa tangu Iran ianze juhudi za kufuatilia namna wananchi wake watakavyokwenda kutekeleza amali ya Hija mwaka huu, lakini viongozi wa Saudia wanaendelea kukataa mapendekezo ya Iran katika masuala kama vile viza, usafiri wa anga na kudhaminiwa usalama wa mahujaji wa Iran, hasa kutokana na kuwa hakuna ubalozi wa Saudia nchini Iran. Ubalozi wa Uswisi unalinda maslahi ya Saudia nchini Iran lakini wakuu wa Saudia wamekattaa mahujaji Wairani wachukue visa kupitia ubalozi huo.

Maafisa wa Taasisi ya Hija ya Iran wanasema kuwa, kwa kuzingatia kwamba, hisa ya Iran ya Hija ni mahujaji 65 elfu na kwa sasa hakuna uhusiano wa kibalozi kati ya Tehran na Riyadh, haitawezekana kwa mahujaji hao kwenda kuchukua viza katika nchi ya tatu. Mbali na hayo, Saudia imetangaza kuwa, hakuna ndege yoyote kutoka Iran yenye haki ya kutua nchini Saudia na kwamba, mahujaji wa Kiirani hawapaswi kushiriki katika marasimu ya kujibari na washirikina katika ibada ya Hija.

Sisitizo la Iran la kulindwa haki, izza na usalama wa mahujaji wake katika ibada ya Hija linatolewa katika hali ambayo, ibada ya Hija mwaka jana iliambatana na matukio machungu ya umwagikaji damu bure bilashi. Katika tukio la kwanza la kuanguka winchi ndani ya Masjidul Haram, takribani mahujaji 180 walipoteza maisha wakiwemo mahujaji wa Kiirani. Aidha kulitokea maafa makubwa huko Mina kutokana na uzembe na usimamizi mbovu wa viongozi wa Saudia na hatua yao ya kufunga njia zinazoelekea katika sehemu ya kumpiga mawe shetani. Maelfu ya mahujaji walipoteza maisha wakiwemo mahujaji 465 wa Kiirani.

Katika mazingira kama haya watawala wa Saudia ambao wanajiita kuwa ni Mahadimu wa Haramu Mbili Tukufu, wakiwa na lengo la kukwepa matokeo mabaya ya kuwazuia Wairani kwenda kufanya ibada ya Hija, wanafanya njama za kuwatwisha mzigo viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3500285
captcha