IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran kutetea taifa linalodhulumiwa la Palestina

18:00 - July 06, 2016
1
Habari ID: 3470435
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo kuwa taifa la Iran litaendelea kusimama kidete dhidi ya maadui wote kwa ajili ya kutetea taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo leo mjini Tehran katika hotuba za Swala ya Idul Fitri na kuongeza kuwa, mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds tena katika kipindi cha joto kali ni dhihirisho la kazi kubwa na jihadi ya Wairani katika mwezi uliomalizika jana wa Ramadhani.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa mahudhurio hayo ya Wairani katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamewatangazia walimwengu kwamba: Japokuwa baadhi ya nchi za Waislamu zinasaliti malengo na mapambano ya Wapalestina, lakini serikali na taifa la Iran liko tayari kusimama kidete mbele ya maadui wote kwa ajili ya Palestina.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni katika nchi kama Iraq, Uturuki, Bangladesh na kwengineko na kusema, magaidi wanaotaka kueneza Uislamu bandia unaoarifishwa na mabwana zao wameifanya Sikukuu ya Idi ya mwaka huu kuwa siku ya maombolezo katika baadhi ya nchi za Waislamu na kwamba uhalifu na jinai hizo ni matokeo ya magaidi waliopewa malezo na mafunzo kupitia vyombo vya usalama vya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesisitiza kuwa lawama za mauaji ya watu wasio na hatia katika nchi za Mashariki ya Kati zinaelekezwa kwa wafadhili na waungaji mkono wao ambao hata wao wenyewe sasa wameanza kupatwa na madhara ya ugaidi huo. Amesema madhambi na makosa hayo hayatasahaulika.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa inasikitisha sana kuona baadhi ya nchi zikiwasha moto wa vita katika nchi kama Syria, Libya na Yemen na kuongeza kuwa: Wananchi wa Yemen wanaendelea kupigwa kwa mabomu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu sasa lakini hatuna budi kuwapongeza watu wa Yemen na uongozi wao wenye busara ambao wamejitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika mazingira hayo na kipindi cha joto kali.

Amesisitiza kuwa mapambano ya kukomboa Palestina ni mapambano ya Kiislamu na ya watu wote.

3513279

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
juma zaililah
0
0
mungu ibariki dunia tuwe na amani
captcha