IQNA

Turathi

Ukurasa wa kale wa Qur’ani Tukufu waondolewa kwenye mnada baada ya kubainika ulikuwa umeporwa

22:02 - October 29, 2023
Habari ID: 3477808
LONDON (IQNA) – Mnada wa Christie umeondoka nakala ya maandishi ya Qur'ani Tukufu kwenye mnada wake baada ya baadhi ya wanaharakati kusema ni sehemu ya Msahafu ulioibwa kutoka kwenye jumba la makumbusho la Iran.

Mnada wa Christie umesema unchunguza madai hayo na kwamba nakala hiyo ya kihistoria haiuzwi tena. Ukurasa huo wa msahafu ni wa karne ya 9 au 10, na una maandishi ya Kufi, moja ya mitindo ya zamani zaidi ya maandishi ya Kiarabu. Uuzaji wa ukurasa huo msahafu ulitaraji kuingiza kati ya £15,000 na £20,000 katika mnada huo.

Hata hivyo, baadhi ya wapenda urithi wa kitamaduni waliibua wasiwasi kwamba ukurasa huo ni za Msahafu ulioporwa kutoka kwenye Jumba la Makumbusho la Pars huko Shiraz, kusini mwa Iran, takriban miaka 20 iliyopita. Jumba hilo la makumbusho lilikuwa na Msahafu adimu ulioandikwa kwa maandishi ya Kufi, na kurasa zake zimekuwa zikuziwa vipande vipande katika minada mbalimbali duniani.

Wizi huo ulitokea Aprili 16, 2003, wakati watu wanne waliofunika nyuso zao waliingia kwenye jumba la makumbusho wakiwa na tikiti, wakashikilia walinzi wakiwa wamewaelekezea bunduki, wakavunja kisanduku cha kuonyesha na kupora Msahafu huo adimu. Gavana wa wakati huo wa Shiraz alithibitisha siku iliyofuata kwamba Msahafu huo ulikuwa umepora na  wezi hawakukamatwa kamwe.

Maandishi ya Kufi yamepewa jina la mji wa Kufah nchini Iraq, ambako iliaminika kuwa yalitokea.

3485776

Habari zinazohusiana
Kishikizo: msahafu kale kufi
captcha