IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/36

Utangulizi wa Kuhusu Historia ya Hati za Qur'ani Tukufu

13:47 - November 26, 2023
Habari ID: 3477949
TEHRAN (IQNA) – Ni jambo linalokubalika miongoni mwa Waislamu na wanazuoni wengi wasio Waislamu yaliyomo katika Qur’ani Tukufu hayajabadilika tangu ilipoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Wanazuoni wengine wasio Waislamu ingawa wamefanya tafiti juu ya historia ya nakala kongwe za hatu au maandishi ya Msahafu (Nakala ya Qur'ani Tukufu0.

Francois Deroche, mwanachuoni wa Kifaransa ambaye ni mtaalamu wa Codicology na Palaeography, amejadili sifa za Misahafu ya awali kabisa katika kitabu chake “Nakala za Kwanza za Qur'ani za Zama za Bani Ummaya: Tathmini ya Kwanza”.

Katika utafiti wake, Deroche anachanganua mitindo ya uandishi katika Misahafu hii ya kihistoria, akizingatia mwandishi wa kaligrafia na eneo ambalo Msahafu ulikotoka.

Anatoa maelezo ya hati-mkono, aina tofauti-tofauti kwenye wino, karatasi, na nyenzo nyinginezo zilizotumiwa humo. Pia anaelezea hatua za maendeleo katika ujuzi wa kaligrafia katika miaka tofauti.

Anasisitiza jukumu la Misahafu hii katika kuthibitisha usahihi wa kile kinachokuja katika maandishi ya Qur'ani Tukufu.

Sehemu ya kwanza ya kitabu hiki imejikita kwenye idadi Misahafu ya zama za Bani Umayya, ambayo aghalabu sasa iko  huko Paris na Saint Petersburg.

Katika sura ya pili ya kitabu, mwandishi anachambua Misahafu mitatu. Mmoja ulio Istanbul, mwingine uko London na wa tatu uko Saint Petersburg.

Pia anazungumzia maandishi ya Misahafu iliyo huko Sana’a ,  Yemen na Kairouan huko Tunisia. Mwonekano wa jumla wa nakala hizi, haswa mtindo wao wa kaligrafia, ni sawa na maandishi ya zamani zaidi ya Quran.

Yawezekana ni ya kabla mwaka  695 Miladia (CE) na wakati wa utawala wa Abdul Malik ibn Marwan (646-705 Miladia).

Katika sura ya tatu, mwandishi anajadili mabadiliko katika muundo wa miswada, akizingatia nakala mbili ambamo kuna mpangilio wima unaoonyesha maendeleo katika miswada.

Katika sura ya mwisho, "Nakala ya Mfalme" (pengine nakala ya Uthmaniya) inachambuliwa na mwandishi.

Deroche pia anarejelea miswada miwili moja katika Sana’a na nyingine nchini Ujerumani, akisema ilitolewa katika kipindi cha enzi ya Umayyad ambapo umakini zaidi ulilipwa kwa uzuri wa nakala hiyo.

Habari zinazohusiana
captcha