IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Hujuma za Chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza zaongezeka mara saba baada ya Vita vya Gaza

18:35 - December 22, 2023
Habari ID: 3478073
IQNA - Kumekuwa na ongezeko mara saba la mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) nchini Uingereza kutoka Oktoba 7 hadi Desemba 13. Hayo ni kwa mujibu wa taasisi ya Tell MAMA ambayo iafuatilia matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza.

Taasisi hiyo iliripoti kesi 1,432 katika kipindi hiki, ikilinganishwa na kesi 195 (153 nje ya mtandao na 42 mtandaoni) mwaka wa 2022. Hili ndio ongezeko la juu zaidi katika ripoti za huduma yao katika siku 68.

Matukio hayo yalijumuisha visa 387 vya tabia ya matusi, vitisho 52, mashambulizi 49, vitendo 46 vya uharibifu, visa 40 vya ubaguzi, vitendo 28 vya matamshi ya chuki, na matukio 11 ya maandishi hidi ya Uislamu.

Mtandaoni, kulikuwa na kesi 819, zikiwemo za michoro ubaguzi wa rangi, wito wa vurugu dhidi ya Waislamu, na nadharia za njama za ubaguzi wa rangi zinazoenezwa na watu wenye msimamo mkali wa wazungu wa mrengo wa kulia.

Kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu kulienda sambamba na vita vya Israel vya mauaji ya halaiki  dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, vilivyoanza Oktoba 7. Vita hivyo pia vilichochea chuki dhidi ya Uislamu katika mataifa mengine ya magharibi.

Kwa mfano, nchini Marekani, mvulana wa Kipalestina Mmarekani anayeitwa Wadea al-Fayoume alidungwa kisu mara 26 na mwenye nyumba mwenye umri wa miaka 71 ambaye inadaiwa alikuwa na hasira kuhusu mzozo wa Israel na Wapalestina.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) na washirika wake kote Marekani pia walirekodi visa zaidi vya ubaguzi dhidi ya Waislamu na unyanyasaji kufuatia vita vya Gaza.

3486510

Habari zinazohusiana
captcha