Likilinukuu gazeti la Qatar la ar-Raya Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa limesema kuwa Batina Abdulllah Abdul Ghani, mkuu wa Taasisi ya Qur’ani ya Doha amesema kuwa lengo hasa la kuandaliwa na kutiwa saini hati hiyo ni kuratibu na kuzifanya ziwe na natija zaidi shughuli za taasisi zote za Qur’ani na uhubiri wa Kiislamu katika kipindi cha mwaka mzima, kwa kuwasilisha mipango ya pamoja ya kuwafundisha Qur’ani watu wa umri na matabaka mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano wa taasisi za Qur’ani. Ameendelea kusema, lengo jingine la hati hiyo ya ushirikiano wa pamoja ni kuunga mkono shughuli za tablighi na uhubiri wa kidini katika nchi zinazopakana na Ghuba ya Uajemi na kuleta mbinu mpya katika shughuli za kuhifadhi na mafunzo ya sunna za Mtume Mtukufu (SAW). Amesema wakuu wa taasisi za Qur’ani watakaoshiriki katika kikao hicho watatoa maoni yao kuhuisiana na mipango inayopaswa kutekelezwa baadaye. Amesema taasisi za Qur’ani za Qatar zilizotia saini hati hiyo ni, az-Zahra, al- Hinziraab, Hajir, Darul Hikma na Jumuia ya Qur’ani Tukufu ya Qatar. 317910