IQNA

Mafunzo ya Qur'ani kwa walinganiaji wa kike wa Marekani

10:45 - December 08, 2008
Habari ID: 1717161
Mafunzo ya muda ya maana ya aya za Qur'ani, misingi na mafundisho ya dini ya Kiislamu makhsusi kwa walinganiaji wa kike kutoka Marekani yataanza tarehe 14 mwezi huu wa Disemba nchini Imarati.
Mafunzo hayo yatakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja yatafanyika katika Taasisi ya Utamaduni na Masuala ya Kiislamu ya Zayid katika mji wa Dubai.
Walinganiaji 21 wa kike kutoka Marekani watashiriki katika mafunzo hayo ya muda.
Mafunzo hayo yatajumuisha elimu ya maana ya aya za Qur'ani, fiqhi ya Kiislamu hususan sheria zinazohusiana na masuala ya wanawake, itikadi za Kiislamu, hadithi na sira ya Mtume (saw) na lugha ya Kiarabu.
Wakiwa nchini Imarati walinganiaji hao wa Kiislamu wa kike kutoka Marekani watatembelea taasisi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya Qur'ani na ya Kiislamu na kuhudhuria kongamano la "Mchango wa Mwanamke wa Kiislamu Katika Maendeleo ya Jamii." 331133

captcha