IQNA

Televisheni ya Qur'ani kwa lugha ya Mabarbari kuanzishwa Algeria

18:11 - March 04, 2009
Habari ID: 1751879
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Algeria amesema kuwa kanali ya televisheni ya Qur'ani kwa lugha ya Tamazight itafunguliwa mwezi ujao.
Ezzedine Mihoubi amesema kuwa kanali hiyo ya televisheni itaanza kutangaza kwa masaa manane kwa siku na kwamba wakati huo utaongezwa kadiri muda unavyopita.
Amesema kuwa miongoni mwa ratiba za televisheni hiyo ni kutoa mafunzo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu, hotuba za maulamaa wa Kiislamu kuhusu matatizo ya jamii ya Kiislamu na vipindi vya kiutamaduni. Lugha ya Tamazight ni mojawapo ya lugha za Mabarbari wanaoishi katika nchi za kaskazini mwa Afrika. 372328

captcha