IQNA

Wanaharakati wa kike wa Qur’ani Iran kuenziwa

17:23 - July 02, 2011
Habari ID: 2147189
Sambamba na Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran, kongamano la pili la kuwaenzi wanawake wanaharakati katika uga wa Qur’ani linafanyika Julai pili.
Kongamano hilo linahudhuriwa na Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami mwanachama wa Baraza la Wataalamu la Iran na Hujjatul Islam Ali Mohammadi mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu na Mkuu wa Shirika la Awqaf na vilevile wataalamu na wanaharakati wa kike wa Qur’ani.
Wanawake 28 ambao wamekuwa na nafasi muhimu katika uga wa Qur’ani wataenziwa.
Kati ya watakaoenziwa ni majaji wa mashindano ya Qur’ani, waalimu wa Qur’ani, wahubiri wa Qur’ani, wanaotengeneza sanaa za Qur’ani, waandishi wa vitabu vinavyohusiana na maarifa ya Qur’ani n.k.
817916
captcha