IQNA

Mwanamke Mwislamu afutwa kazi Marekani kwa ajili ya kuvaa Hijabu

9:03 - August 07, 2016
Habari ID: 3470501
Mwanamke Mwislamu nchini Marekani amefutwa kazi baada kutokana na kuvaa vazi la Hijabu akiwa kazini.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bi. Najaf Khan alikuwa akifanya kazi katika kituo kimoja cha tiba ya meno mjini Viriginia huko Marekani. Bi. Khan anasema kuwa, msimamizi wake kazi alimfahamisha kuwa Hijabu yake kazini ni kero wagonjwa wanokuja katika kituo hicho kwa matibabu ya meno hivyo hapaswi Hijabu akiwa katika mazingira ya kazini.

Mwanamke huyo Mwislamu amebaini kuwa, mkurugenzi wake alimtishia akimwambia kwamba, kama ataendelea kuvaa vazi hilo la stara ya mwanamke wa Kislamu katika mazingira ya kazini, atapoteza kazi yake.

Bi Najaf Khan aliongeza kuwa: 'Sikudhani kabisa kama uvaaji wangu wa kujisitiri kwa vazi la Hijabu ungekuwa ni jambo kubwa kiasi hicho na hata nilipoambiwa nisivae Hijabu nikiwa kazini nilijua ni kama ombi lakini katu sikudhania kwamba, kama sitatii amri hiyo ambayo kimsingi inakinzana na mafundisho ya dini yangu, basi ningepoteza kazi yangu.'

Wakati huohuo Baraza la Mahusiano ya Kiislamuna Marekani(CAIR) limekitaka kituo hicho cha tiba ya meno mjini Viriginia kumrejesha kazini mara moja mwanamke huyo na kumlipa gharama za kisaikolojia na kinafsi kilizomsababishia.

Mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuwa, hakuna mfanyakazi yeyote ambaye anapaswa kufukuzwa kazi kutokana na kushikamana na misingi ya dini yake.

Wakati hayo yakijiri, ripoti yamwezi Juni mwaka huu ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Berkeley jimboni California ilifichua kuwa, mashirika yapatayo 74 yametoa kiasi cha dola milioni 206 za Marekani kwa ajili ya kutumika kueneza chuki na hofu dhidi ya Uislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa Idara ya Masuala ya Umma ya Waislamu MPAC, mjini Washington DC, jamii za Waislamu kote Amerika Kaskazini inakabiliwa na hujuma za wanaopinga Uislamu na Waislamu.

3460614

captcha