IQNA

Msikiti wateketezwa moto kabla ya Sala ya Idul Adha Marekani

12:26 - September 13, 2016
Habari ID: 3470561
Kituo cha Kiislamu katika jimbo la Florida Marekani kimeteketezwa moto na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kituo cha Kiislamu katika eneo la Fort Pierce, Kaunti ya St Lucie kilitetekea moto Jumatatu wakati Waislamu walikuwa wanajitayarisha kusherehekea Siku Kuu ya Idul Adha.

Moto huo mkali uliharibu paa la ukumbi asili wa msikiti na polisi wanasema wanamtafuta mtu aliyetambuliwa kuwa 'Mzungu mwenye asili ya Kihispania' ambaye ni mshukiwa mkuu wa hujuma hiyo.

Kitendo hicho kimelaaniwa na Waisalmu wa Marekani ambao wamebainisha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka vitendo vya chuki dhidi yao.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) limesema vitendo kama hivyo vimepelekea Waislamu kukabiliwa na wasi wasi mkubwa kwani hawajui ni wapi na ni lini watashambuliwa, Msemaji wa CAIR mjini Florida Wilfredo Amr Ruiz amesema Waislamu wamesikiishwa na hujuma hiyo iliyojiri wakikaribia kusherehekea siku kuu yao kubwa zaidi. Hujuma hiyo ilisadifiana na kumbukumbu ya mwaka wa 15 tokea yajiri mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 jambo ambalo limepelekea maafisa wa usalama waanzishe uchunguzi kubaini iwapo kuna uhusiano wa matukio hayo mawili.

Waislamu nchini Marekani wanakabiliana na wimb kubwa la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia hata baada ya kuwa wanalaani ni vikali hujuma ya kigaidi ambazo zinabasibishwa na watu wanaodaiwa kuwa Waislamu.

3529764

captcha