IQNA

Waislamu Nigeria waandamana wakielekea Abuja kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

18:20 - September 23, 2016
Habari ID: 3470577
Waislamu wa Nigeria kwa mara nyingine tena wameandamana wakimuunga mkono Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria anayeshikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo kwa miezi kadhaa sasa.

Maelfu ya Waislamu Alhamisi walifanyamaandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya kumuunga mkono mwanazuoni huyo wa Kiislamu. Waandamanaji hao walitoa wito wa kuachiliwa huru mwanaharakati huyo wa Kiislamu anayeshikiliwa na vyombo vya usalamakwa miezi kadhaa sasa bila ya kufunguliwa mashtaka.

Waandamanaji hao walifanya harakati kuelekea mji mkuu Abuja na kusisitiza kwamba, wanataka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky, mke wake pamoja na Waislamu wengine wa Kishia wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama vya Nigeria.

Hata hivyo maandamano hayo yalizimwa na vikosi vya usalama ambavyo viliingilia kati na kuwatawanya waandamanaji hao. Ripoti zinaeleza kuwa, maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Ibrahim Zakzaky yameongeza mno Nigeria katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo, jumuiya za kutetea haki za binadamu zimekuwa zikikosoa na kulalamikia miamala iliyo dhidi ya binadamu ya jeshi na askari usalama wa Nigeria dhidi ya Waislamu wa Kishia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Disemba mwaka jana 2015, siku moja baada ya jeshi la Nigeria kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria.

Ikumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.

Aidha Jeshi la Nigeria lilimkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake. Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inaripotiwa kuwa mbaya huku taarifa zikisema amepoteza jicho moja mbali na majeraha mengine mwilini. Serikali ya Nigeria inamshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu tokea Desemba mwaka jana pasina kumfungulia mashtaka.

3532238

captcha