IQNA

Annan awasili Myanmar kuchunguza ukatili dhidi ya Waislamu wa Rohingya

19:13 - December 02, 2016
Habari ID: 3470710
IQNA-Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan yuko nchini Myanmar kuchunguza ukatili wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Annan na timu yake waliwasili leo Ijumaa katika Jimbo la Rakhine, eneo ambalo wiki iliyopita jeshi liliwaua Waislamu 86, kwa mujibu wa takwimu za serikali. Wachunguzi huru wanasema Waislamu zaidi ya 400 waliuawa kiholela.

Anan ameteuliwa na kiongozi asiye rasmi wa Myanmar Aung San Suu Kyi kuchunguza mauaji ya Waislamu wa Rohingya.

Suu Kyi ambaye anapigiwa debe na nchi kuwa eti ni 'nembo ya demokrasia' amelaumuwa vikali kwa kutochukua hatua yoyote ya maana kuwalinda Waislamu wa Rohingya ambao mashirika ya haki za binadamu yanasema wanaagamizwa kwa umati na jeshi.

Kwa mtazamo wa wananchi wa Myanmar, kama kweli Bi Suu Kyi ana nia ya kweli ya kuimarisha utawala wa sheria na kuleta utulivu nchini Myanmaar, anapaswa achukue hatua za kivitendo za kuwatia mbaroni wahusika wa mauaji ya Waislamu wa Rohingya kama hatua ya awali ya kuleta utulivu na kuimarisha umoja wa kitaifa nchini Myanmar.


Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraiaWaislamu ambao idadi yaoni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesiakutokana na mashambulio ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3550264

captcha