IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Waislamu wa Uholanzi wazinuda kampeni ya 'Usiichome Qur’ani, Isome’

22:04 - February 12, 2024
Habari ID: 3478342
IQNA - Waislamu wa Uholanzi wamesambaza nakala za Qur’ani Tukufu zenye tafsiri ya Kiholanzi ili kujibu la jaribio la mrengo mkali wa kulia la kuchoma kitabu kitakatifu cha Waislamu mwezi uliopita.

Hafla hiyo inayoitwa "Usichome, Soma", iliandaliwa na viongozi sita wa misikiti huko Arnhem, mji ulioko mashariki mwa Uholanzi.

Tukio hilo lilifanyika katika viwanja vya Jansplein Square, ambapo Edwin Wagensveld, kiongozi wa kundi linalopinga Uislamu la Pegida, alijaribu kuchoma moto nakala ya Qur’ani mnamo Januari 13. Waandalizi pia walitoa vipeperushi vinavyoelezea mafundisho Uislamu kwa umma.

Galip Aydemir, rais wa Wakfu wa Msikiti wa Arnhem Türkiyem, ambao unashirikiana na Wakfu wa Diyanet wa Uholanzi, alisema wanataka kuwaonyesha watu kwa nini Uislamu na Quran ni takatifu kwa Waislamu.

Vile vile ametoa wito wa umoja na mshikamano baina ya watu wa Arnhem akisema: "Qur'an na maandiko matukufu yote yasichomwe moto, bali yasomwe."

John Maters, raia wa Uholanzi aliyepokea nakala ya Qur'ani kama zawadi, alipongeza tukio hilo na kulaani kitendo cha Wagensveld. "Unapofikiria juu ya kitendo cha uchochezi kilichofanywa mwezi uliopita, unageuza watu kuwa maadui dhidi ya kila mmoja. Sidhani kama unapaswa kuwa wa kidini ili kuelewa kwamba hii haina maana yoyote," alisema.

Wagensveld ina rekodi ya matukio ya uchomaji wa nakala za Qur’ani  Tukufu  katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Aliinajisi nakala ya Qur’ani Tukufu mbele ya jengo la muda la bunge la Uholanzi huko The Hague na katika maandamano ya peke yake huko Utrecht mnamo 2022 na 2023. Pia alikamatwa huko Rotterdam na The Hague kwa kujaribu kuchoma nakala ya Qur’ani bila kufuata sheria za maandamano. Katika visa vyote viwili, vikundi vya Waislamu vilifanya maandamano ya kupinga hatua ya Pegida. Mwaka jana, Wagensveld pia alirarua nakala ya Qur’ani Tukufu mbele ya Ubalozi wa Uturuki huko The Hague.

3487159

Kishikizo: qurani tukufu uholanzi
captcha