IQNA

Maonyesho ya Kaligrafia ya Qur'ani Tukufu yamezinduliwa katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Maonyesho hayo yana aya za Qur'ani ambazo zimeandikwa katika kipindi cha miaka 45 iliyopita na Ustadh Sahmudin Zamani. Maonyesho hayo yalifunguliwa Jumanne 7 Mei katika Ukumbi wa Khayal wa Taasisi ya Sabaa.