Picha: Kituo cha Metro cha Maria Mtakatifu chafunguliwa Tehran
IQNA – Kituo cha metro (treni ya chini ya ardhi) cha Maryam-e Moghaddas (Bikira Maria Mtakatifu) kimezinduliwa rasmi tarehe 29 Novemba 2025 jijini Tehran. Ndani ya kituo kipya, wageni wanakutana na kazi za sanaa zenye maudhui ya Kikristo na taswira ya Bikira Maria, pamoja na vipengele vya kimaono na vya usanifu vilivyochochewa na miundo ya makanisa na kuchanganywa na mitindo ya Kipersia.