Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa serikali, maafisa wa kijeshi, na umati mkubwa wa wananchi, likiwa ni ishara ya heshima na kumbukumbu kwa viongozi waliotajwa kuwa na mchango mkubwa katika harakati za mapambano ya Kiislamu. Hafla hiyo ilijumuisha kisomo cha Qur'ani, hotuba za viongozi wa kidini na kisiasa, pamoja na maonyesho ya picha na video za kihistoria zinazohusiana na maisha na harakati za mashahidi hao.
.