IQNA

Sherehe za kufungua mpango mkubwa zaidi wa kusomesa Qur'ani Tukufu nchini Iraq katika msimu wa majira ya joto zimefanyika Ijumaa 26 Julai mjini Karbala. Mpango huo unasimamiswa na Haram ya Hadhrat Abbas unajumuisha wanafunzi 22,000 kutoka mikoa mbali mbali ya Iraq.