IQNA

Msafara wa Qur'ani ambao ni maarufu kama 'Msafara wa Nuru unajumuisha wasomaji Qur'ani Tukufu ambao aghalabu ni kutoka Iran. Walio katika msafara huo wameandamana na waumini wanaoshiriki katika ibada ya Hija na wanasoma Qur'ani katika vikao mbali mbali na pia katika maeneo matakatifu katika ardhi ya Wahyi. Hapa chini ni qiraa ya baadhi ya wasomaji Qur'ani katika Msafara wa Nuru.