IQNA

Hafla ya kubadilishwa bendera ya Haram ya Sayyid Abduladhim al Hassani AS

Hafla ya qiraa ya pamoja ya wahudumu na ubadilishaji bendera ya Haram ya Sayyid Abduladhim al Hassani AS imefanyika katika usiku wa Wilada ya Mtukufu huyo Jumamosi katika eneo hilo takatifu kusini mwa Tehran.
Tarehe 4 Mfunguo Saba Rabiuth-Thani  miaka 1268 iliyopita, alizaliwa Sayyid Abdul Adhim al Hassani, mmoja wa wajukuu wa Imam Hassan al Mujtaba AS huko katika mji wa Madina. Sayyid Abdul Adhim alikuwa mmoja kati ya shakhsiya walioaminiwa na Imam al Hadi AS na alinukuu hadithi moja kwa moja kutoka kwa maimamu watukufu kama vile Ridha, Jawad na al Hadi AS. Sayyid Abdul Adhim alihamia Iran kutokana na pendekezo la Imam al Hadi AS kwa ajili ya kuwaongoza Waislamu na akaishi katika mji wa Rei karibu na Tehran ya sasa. Sayyid Abdul Adhim aliuawa shahidi mwezi Shawwal mwaka 250 Hijria. Kaburi la mtukufu huyo liko katika eneo la Rey kusini mwa Tehran na ni miongoni mwa maeneo yanayotembelewa sana na Waislamu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.