IQNA

Baada ya shughuli ya mazishi na kuusindikiza mwili mtoharifu wa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wapiganaj jihadi wenzake katika miji ya Kadhimein, Karbala, Najaf nchini Iraq na kisha nchini Iran katika mji mtakatifu wa Mashhad, Tehran na Qum, leo 7 Januari mji wa Kerman umempokea mwili wa mwenyeji wake shujaa, Haj Qassem kwa ajili ya mazishi na maziko katika makaburi ya mashahidi mjini humo.