IQNA

Msikiti wa Jamia wa Ul-Alfar nchini Sri Lanka, ambao miongoni mwa watu wa eneo hilo unajulikana kama Samman Kottu Palli kwa maana ya Msikiti Mwekundu, uko katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo na ni moja kati ya misikiti mikongwe zaidi mjini humo mbali na kuwa kivutio cha utalii. Ujenzi wa msikiti huo ulikamilika mwaka 1908 Miladia.