IQNA

Kufuatia hatua ya Saudi Arabia ya kusitisha kwa muda raia wa kigeni kuingia nchini humo kwa ajili ya Ibada ya Umrah mjini Makka na Ziyara katika Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina ili kuzuia kuenea na kirusi cha Corona, hali katika Al Kaaba Tukufu na Al- Masjid Al-Haram ni ya kipekee kwani hakujawahi kushuhudiwa watu wakiwa wachache kiasi hiki katika eneo hilo takatifu.