IQNA

Kaburi la Saadi mjini Shiraz

Saadi wa Shiriaz ni malenga, mshairi na mwalimu stadi wa tungo za mashairi na nathari wa lugha ya Kifarsi. Alizaliwa mwaka 1210 Miladia na kufarikia mwaka 1291. Saadi Shirazi ni miongoni mwa malenga na washairi wakubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Saadi Shirazi ameandika vitabu kadhaa, muhimu zaidi ni kile cha tungo cha Bustan na kitabu chake cha nathari cha Golestan.

Kaburi au ziara lake ambalo linajulikana kama Saadiyeh liko katika mji wa Shiraz, kusini mwa Iran na limejengwa kwa usanifu majengo wenye mvuto mkubwa.